Simu nyingi zinazotumia mfumo wa android huwa zinakuwa na recovery mode. Kama jina livyosema " Recovery " hii ni sehemu muhim...
Simu nyingi zinazotumia mfumo wa android huwa zinakuwa na recovery mode. Kama jina livyosema "Recovery" hii ni sehemu muhimu sana kwenye simu yako na inakupa uwezo wa kurekebisha simu yako endapo itakuwa inakupa matatizo madogo madogo.
Kwa mfano, Samsung Galaxy S3 inakuja na recovery na jinsi ya kuingia kwenye recovery kwenye Samsung galaxy s3 ni rahisi sanaa. Kuingia kwenye recovery mode haiwezi kuleta madhara yoyote kwenye simu yako bali utakuwa umeijua simu yako kiundani zaidi.
JINSI YA KUINGIA KWENYE RECOVERY KWA WALE WANATUMIA SAMSUNG GALAXY S3 NA SIMU NYINGINE ZA SAMSUNG
1) Zima simu yako (Power off your device).
2)Shikilia cha kuongeza sauti (vol up) + Home (cha katikati) + Cha kuwashia (power) kwa muda wa kama wa sekunde tano kisha achia cha kuwashia huku ukiwa umeendelea kushikilia cha kuongeza sauti (vol up) + Home (cha katikati).
Baada ya muda mfupi utaona screen yako inaoneka kama hapo kwenye picha chini.
Tumia cha kuongeza na kupunguza sauti kwenda kwenye menu unayoitaka. Kisha bonyeza cha kuwashia kuchagua menu yako.
Endapo utashindwa na utahitaji msaada kuhusiana na tatizo lolote kwenye simu yako ya andorid basi wasiliana nasi kwa kutumia WhatsApp namba +255 713 515 059. Pia unaweza ku-like Facebook Page yetu iitwayo
COMMENTS