Jinsi Ya Ku-Root Huawei Y300 Na Unlock Bootloader

Huawei Y300 ni simu nzuri ambayo inaweza kufanya mambo mengi licha ya kuwa bei nafuu. Uzuri huo wa huawei y300 huongezeka pale utakapo ...


Huawei Y300 ni simu nzuri ambayo inaweza kufanya mambo mengi licha ya kuwa bei nafuu. Uzuri huo wa huawei y300 huongezeka pale utakapo root simu yako na ku-unlock bootloader.

Endapo utafanikiwa ku-unlock bootloader na ku-root huawei Y300 basi utaweza kufanya yafwatayo;-



  1. Kuweka custom rom mbali mbali kama slimkat inayo tumia android 4.4.4
  2. Utaweza kuweka Exposed framework ambayo itakusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako
  3. Utaweza kuweka bootanimation tofauti 
Hizo ni baadhi ya faida ambazo utapa endapo uta root na ku unlock bootloader. Sasa tuangalie ni jinsi gani utaweza ku-unlock bootloader na root huawei Y300

VIGEZO NA MASHARTI VYA KUZINGATIA KABLA UJA ROOT NA KU-UNLOCK BOOTLOADER

  1. SISI HATUTAHUSIKA ENDAPO UTAARIBU SIMU YAKO
  2. HAKIKISHA UNA UWELEWA KIDOGO WA COMPUTER
  3. GENERAL COMMON SENSE IS REQUIRED
  4. WINDOW PC
JINSI YA KU UNLOCK BOOTLOADER, ROOT NA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE HUAWEI Y300

STEP 1

Download HuaweiY300v1.1.exe        DOWNLOAD 
NOW.   Kisha install kwenye computer yako

STEP 2  

Baada ya ku-install program nenda kwenye local disk kisha hakikisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO lipo ndani ya program files na sio program files(x86). Kama lipo ndani ya 
program files(x86) hakikisha unalipeleka (move) kwenye program files. Endapo hutafanya hivyo basi program yako haitafanya kazi




STEP 3

Baada ya kuliamisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO kwenda program files, lifungue hilo folder kisha ndani utakuta mafolder matatu. Fungua folder linaloitwa tools kisha utaona mafolder mawili. Fungua folder linaloitwa unlocktools kisha utaona mifile yafutayo





STEP 4
Double click program inayoitwa HuaweiY300 ambayo ipo ndani ya unlocktools folder na kisha click button inayoitwa Install driver ambayo ipo kushoto juu kabisa


  

STEP 5
Kwenye simu yako nenda kwenye setting kisha developer options na tick kibox kinachosema USB DEBUGGING (debug mode when usb is connected)

STEP 6

Zima simu yako ya huawei y300 kisha toa battery suburi kama 5sec kisha rudisha battery halafu bonyeza na kushikilia kitufe cha kupunguza sauti (vol down) kisha bonyeza cha kuwashia (power button) huku ukiwa umeendelea kushikilia kitufe cha kupunguza kisha subiri kama 10sec huku ukiwa bado umeshikilia kitufe cha kupunguza sauti (vol down) kisha achia kitufe cha kupunguza sauti (vol down). Simu yako itaonyesha logo ya huawei lakini haitawaka. Chomeka usb cable kwenye computer na simu yako. 


STEP 7
Bonyeza Kitufe kinachosema check bootloader status(kipo upande wa kulia juu kabisa). Program yako itakuonyesha kama bootloader yako ipo locked or unlocked. Picha chini inaonyesha simu yangu ipo unlocked kwa maana tayari nimesha unlock bootloader kwenye simu yangu ya huawei y300.



STEP 8
Kama program itasema bootloader lock status : LOCKED. Bonyeza herufi yeyote kwenye computer yako na simu yako ita reboot. Au chomoa usb kisha toa battery halafu rudishia kisha washa simu yako.


  • kwenye simu yako piga namba hii  *#*#1357946#*#*  ili kupata product ID kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu
  • kwenye simu yako nenda  (Settings -> About phone -> Status)  kisha tafuta IMEI number kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu
  • Zima simu yako kisha toa battery kisha tazama  serial number S/N ya simu yako kisha copy hiyo namba kwenye notepad au andika sehemu.
  • Juu kabisa utaona sehemu wameandika model ya huawei yako. Copy hiyo model sehemu. Model ambazo zinafaa kuwa unlocked ni Y300-0151 na Y300-0100 na Y300-0000. Kama simu yako ni moja ya hizo model nilizotaja unaweza kuendelea step 9

STEP 9

Tembelea hii site http://emui.huawei.com/en/plugin.php?id=unlock&mod=detail
kisha utaona  unatakiwa ujiandikishe kwanza ndipo utakapoweza kupata form kama picha inavyo onekana chini.


Jaza viboksi vyote kisha bonyeza button inayosema submit ambayo ipo kwa rangi nyekundu. Baada ya kubonyeza submit chini kabisa utaona umepewa unlock code ya simu yako na itakuwa imeandikwa kwa rangi nyekundu. Copy hiyo unlock code sehemu kwa maana utaitaji kwenye step 10


STEP 10

Rudia kama ulivyofanya kwenye STEP 6. Kwenya program yako bonyeza button inayosema 1 Unlock bootloader. Kisha andika ile unlock na bonyeza Enter. utaona picha inayofanana na hii. 


 Press enter au any key kwenye computer yako ili uweze ku unlock bootloader. Baada ya hapo utakuwa umefanikiwa ku unlock bootloader ya simu yako ya huawei y300.

STEP 11

Kipengele hichi ni kama unapenda kuweka custom recovery kwenye huawei yako. Custom recovery ni njia moja muhimu inayokuwezesha kuweka custom rom kwenye simu yako.
Kama unataka kuweka custom recovery  hakikisha unazima simu yako. Rudia step 6.

Kwenye program yako bonyeza button inayosema 2 install recovery na utaona picha kama inavyoonekana chini



Press Enter mara mbili au key yoyote mara mbili kwenye computer yako ili uweze kuweka custom recovery. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Kuakikisha kama umefanikiwa kuweka custom recovery unatakiwa uzime simu yako kisha bonyeza cha kuwashia pamoja na cha kuongezea sauti kwa pamoja na vishikilie mpaka utakapoona display yako inaonyesha kama picha chini


Hadi hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Bonyeza kipengele cha reboot na simu yako itawaka kama kawaida.

STEP 12

Kipengele hichi ndio cha mwisho na kinaelezea jinsi ya ku root huawei.  Kwenye program yako bonyeza button inayosema 3 super user(Root) kisha itafunguka new window ambalo ndani yake kuna file linaitwa SuperSU-v1.86. Copy hilo file kwenye memory card ya simu yako. Kisha zima simu yako na tazama video chini jinsi ya kuendelea.



Endapo utashindwa na utahitaji msaada  kuhusiana na tatizo lolote kwenye simu yako ya andorid basi wasiliana nasi kwa kutumia WhatsApp namba +255 713 515 059. Pia unaweza ku-like Facebook Page yetu iitwayo JaBi Technologies

COMMENTS

Name

COMPUTER TIPS,8,IT Darasa,1,Makala,1,Maujanja ya Simu,22,Teknolojia,4,
ltr
item
WaiTech IT Solutions: Jinsi Ya Ku-Root Huawei Y300 Na Unlock Bootloader
Jinsi Ya Ku-Root Huawei Y300 Na Unlock Bootloader
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbTj1rP0K355UUTxOYQjhB0ZL0ygUvVM-lZ2ZkNiqdCAFs-FGeYOpMwKwhaU7uMDmSYyGT6wD1nrXDRpTjvVF6QXjKCqJ6sqnlXbBL-XsqWOYr_TvOBQpQzB4k_Pi44jgw9vcNzHEIfejl/s1600/huawei-y300.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbTj1rP0K355UUTxOYQjhB0ZL0ygUvVM-lZ2ZkNiqdCAFs-FGeYOpMwKwhaU7uMDmSYyGT6wD1nrXDRpTjvVF6QXjKCqJ6sqnlXbBL-XsqWOYr_TvOBQpQzB4k_Pi44jgw9vcNzHEIfejl/s72-c/huawei-y300.jpg
WaiTech IT Solutions
http://waitechs.blogspot.com/2016/10/jinsi-ya-ku-root-huawei-y300-na-unlock.html
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/2016/10/jinsi-ya-ku-root-huawei-y300-na-unlock.html
true
6135567013369675355
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy