UTANGULIZI: Bluetooth ni teknologia ya masafa mafupi ambayo ni rahisi na salama kuitumia kwa maana ya kwamba sio rahisi mtu kuingilia m...
UTANGULIZI:
Bluetooth ni teknologia ya masafa mafupi ambayo ni rahisi na salama kuitumia kwa maana ya kwamba sio rahisi mtu kuingilia mawasiliano ya bluetooth (secure).
Ni teknologia inayotumika kwenye vifaa vingi sana vya kielektroniki, kuanzia simu za mikononi, kompyuta, printa, kwenye vifaa vya burudani na kwenye vifaa vya matibabu.
Kifaa kinachotumia teknologia hii kinaitwa Bluetooth radio. Picha ya hapa chini inaonyesha Bluetooth radio ya nje ya kompyuta ya USB!
USB Bluetooth radio
HISTORIA:
Jina Bluetooth limetoholewa kutoka jina la mfalme wa Denmark na Norway mfalme Harald Bluetooth! Mfalme huyu alitawala miaka ya 936 mpaka 940. Anajulikana sana ka jitihada zake za kuunganisha makabila mbalimbali ya maeneo hayo! Ni kwa kuangalia jitihadi zake, teknologia hii imepewa jina hili la Bluetooth kwa kuwa nayo imelenga kuunganisha vifaa mbalimbali vya kielektroniki.
Logo ya Bluetooth


Teknologia hii ilibuniwa na Bluetooth Consortium mwaka 1998. Consortium hii ilijumuisha kampuni za EricsonIBM, Intel, Motorola, Nokia na Toshiba.
Mwaka 1999, makampuni ya 3Com, Lucent Technlogies na Microsoft yalijiunga na waanzilishi.

HABARI ZA KIUFUNDI (TECHNICAL SPECIFICATIONS):
Teknologia ya Bluetooth inatumia bendi ambayo ni ya bure (ISM band, Unlicensed Frequency) ya 2.4GHz. Vifaa vinaeza kutumia Bluetooth kuwasiliana kama umbali kati ya vifaa hivyo si zaidi ya mita 100. Umbali huu ni kwa [class 1 radios]! kwa class 2 radios ni mita 10 na kwa class 3 radios ni mita 1.
Kasi ya Bluetooth ni kwenye 108.8kbps pande zote (both directions).
PICHA ZA BAADHI YA VIFAA VIANAVYOTUMIA KIFAA CHA BLUETOOTH :

earphone

spika
.jpg)
dashibodi ya gari

Kompyuta
Kwa kuendelea kupata habari zaidi kuhusiana na teknolojia mbalimbali, ungana nasi kwa ku-like Facebook Page yetu iitwayo
COMMENTS