Aina Nne (4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako

Kila mmoja wetu bila shaka anaifahamu hofu aliyonayo. Zipo hofu zile ni za kawaida ambazo zipo ndani ya mtu na kila mmoja anayo. Kwa mfan...


Kila mmoja wetu bila shaka anaifahamu hofu aliyonayo. Zipo hofu zile ni za kawaida ambazo zipo ndani ya mtu na kila mmoja anayo. Kwa mfano mtoto akiwa peke yake mahali penye giza ni lazima aogope, pia ipo mifano mingine mingi kama hiyo.

Lakini leo nataka tujadili aina zingine za hofu ambazo zinatengenezwa na watu wengine katika jamii zetu, pia zipo aina nyingine za hofu ambazo tunazitengeneza sisi wenyewe kutokana na vile tunavyoona mambo ambayo yanatuzunguka.

Hofu hizi ndizo zinazotuzuia kuwa na maisha mengine ya utofauti. Mwisho wa siku tunajikuta ni watu wa kuishi maisha ya vilevile kila wakati. Hata hivyo katika hali hiyo huenda ukawa unalaumu sana ukisema labda unashindwa kufanikiwa zaidi kwa sababu una changamoto ya pesa au sababu wewe ni yatima, mjane au umezaliwa katika familia maskini.

Inawezekana ya kwamba unaona ya kwamba Sababu hizo zina uzito sana na zimechangia wewe kuwa hapo ulipo. Ila ukweli ni kwamba moja ya chanzo kikubwa kilichosababisha wewe kuwa katika hali ya chini ni HOFU iliyopo ndani yako ambayo umeitengeza mwenyewe.
Zifuatazo ndizo aina za hofu zinazotufanya tushindwe kufikia malengo yetu.

1) HOFU YA KUKOSOLEWA.

Watu wengi wamebaki na maisha yale yale ya kila siku kwa sababu ya hofu hii ya kokosolewa. Watu wengi wamekata tamaa ya kuendelea kufanya jambo fulani kwa sababu ya kuna watu waliwakosoa kwa jambo ambalo walikuwa wanafanya. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wana kipaji cha kuimba na katika hilo wapo wengine hupeleka nyimbo zao stesheni mbalimbali za radio na pindi wanapoambiwa kuwa nyimbo zao ni mbaya huwa wanakata tamaa na hiyo ndiyo hofu ya kukosolewa.

Vivyo hivyo hata katika biashara watu wamekuwa wakiambiwa na watu wengine wamekuwa ya kwamba huwezi kufanya hivyo na kwa kuwa mtu anakuwa ana hofu hiyo ya kukosolewa ana amini na mwisho wa siku anaacha kufanya jambo fulani. Pia ikumbwe ya kwamba hii ndiyo sumu kubwa ambayo inaua ndoto za watu wengi sana. Ila kumbuka aina hii ya hofu ndiyo yenye mafanikio makubwa sana mbeleni.

2) HOFU YA KUZEEKA NA KUFA.

Kuna baadhi ya watu wanataka mafanikio ya muda mfupi huku wakiwa na imani kubwa ndani yao kwamba Mafanikio ya muda wa kusaka mafanikio kwa muda mrefu haiwezekani kwa sababu inawezekana wakafariki au wakazeka. Mtu unamwambia matokeo ya jambo hili ni baada ya miaka ishirini kwa kuwa mtu huyo ana hofu atamsikia nikifa je?

Mwingine anapoelezwa jambo hilo utamsikia anasema aaah nitakuwa nimezeeka. Kwa mifano hiyo utakuwa umegundua hofu hizo ni kwa jinsi gani umekuwa unahairisha kufanya mambo fulani ya kimafanikio huku ukihofia aina hizo za hofu. Ili kuondokana na hali hiyo daima kumbuka ishi kama utakufa kesho ila jifunze vitu vingi kama utaishi milele.

3) HOFU YA KUSHINDWA.

Aina ya hofu hii imekuwa inatatesa wengi. Kimsingi ni kwamba kabla ya kuamua kufanya jambo fulani akili yako imekuwa inawaza juu ya jambo hilo. Ila kutokana na kuamua kwako kila ukiwaza juu ya utekelezaji wa jambo hilo unapata majibu mbalimbali ambayo yanakwambia hutaweza. Na kwakuwa unaona ya kwamba utekelezaji wake ni mgumu unaanza kuwaza kwamba jambo hilo ni gumu kwako.
Hivyo unaachana na kufanya  jambo hilo. Pia wapo baadhi ya watu wao huamini ya kwamba wao ni wa kushindwa tu kwa kuwa kila mara kadhaa wamekuwa wanafeli sana. Wito wangu kwako ni kwamba achana mara moja na hofu ya kushindwa amini wewe ni zaidi ya mshindi katika jambo lako.
Soma; Hasara Kubwa Za Hofu Katika Maisha Na Mafanikio Yako.

4) HOFU YA KUWASAIDIA WENGINE.

Tupo baadhi ya watu tumekuwa ni watu wa binafsi sana katika kuwasaidia wengine. Tumekuwa ni watu wakutofundisha watu wengine, huku tukiamini ya kwamba kufanya hivyo ni tutaibiwa mawazo yetu na sababu nyingine kama hizo, huku tukiamini kufanya hivyo ni kuwanufaisha wengine na kuzidi kuamini ya kwamba watatuzidi kiutalaamu. Ila nikwambie kumsaidia mwingine ni jambo jema sana pia kumbuka kuwa wewe ni origino hata akifanya hawezi kuwa kama wewe. Hivyo ni wakati wako muafaka wa kuua aina hiyo ya hofu na kuwasaidia wengine.

MWISHO.

Kupata Makala Mbalimbali na ujuzi kuhusu teknologia mbalimbali  ungana nasi kwa ku-like Facebook Page yetu, ku-like "Click hapa".

COMMENTS

Name

COMPUTER TIPS,8,IT Darasa,1,Makala,1,Maujanja ya Simu,22,Teknolojia,4,
ltr
item
WaiTech IT Solutions: Aina Nne (4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako
Aina Nne (4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitQki5H6thkvNr_HgJrQZXh3sXna3GIsh-AcUbTFdEU_iM2RuFnn4ymdLjKtLIdimh8EsOQgW8yYnSsYXEM_XcljolCqvxLuy_4YiJtCkk57jHs_CLal8POjBR0bzR3EzBFy8djjcmVVU/s1600/Climbing-Mountain.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitQki5H6thkvNr_HgJrQZXh3sXna3GIsh-AcUbTFdEU_iM2RuFnn4ymdLjKtLIdimh8EsOQgW8yYnSsYXEM_XcljolCqvxLuy_4YiJtCkk57jHs_CLal8POjBR0bzR3EzBFy8djjcmVVU/s72-c/Climbing-Mountain.jpg
WaiTech IT Solutions
http://waitechs.blogspot.com/2016/12/aina-nne-4-za-hofu-zinazokukwamisha.html
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/2016/12/aina-nne-4-za-hofu-zinazokukwamisha.html
true
6135567013369675355
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy