Kampuni Ya Apple Kuunda Magari Yatakayojiendesha Yenyewe

  Kampuni ya Apple imetangaza mipango yake ya kuunda magari yanayojiendesha. Kampuni hiyo imekiri hayo kwa mara ya kwanza kwenye barua k...


 
Kampuni ya Apple imetangaza mipango yake ya kuunda magari yanayojiendesha. Kampuni hiyo imekiri hayo kwa mara ya kwanza kwenye barua kwa wasimamizi wa uchukuzi Marekani. Apple imesema inafurahishwa sana na uwezo wa mifumo ya kutumia kompyuta kwenye maeneo mengi, "ikiwemo uchukuzi".

Kampuni hiyo imesema kuna manufaa mengi ambayo yatapatikana kijamii kutoka kwa magari yanayojiendesha.Kumekuwa na uvumi kwa muda kuhusu mipango ya kampuni hiyo, inayofahamika sana kwa kuunda simu za iPhone na kompyuta, kuunda magari yanayojiendesha.Hata hivyo, kampuni hiyo ilikuwa haijakiri hadharani mipango hiyo.

Hata hivyo, kampuni ya Ford, ambayo pia ina mipango ya kuunda magari kama hayo, ambayo inadhamiria yataweza kutumiwa barabarani mwaka 2021, ilisema inaendelea na mpango wake ikifahamu kwamba Apple nao wanaunda magari kama hayo.

Tayari Apple imesajili anwani za tovuti mtandaoni ambazo zinahusiana na magari, zikiwemo apple.car na apple.auto.Google tayari inafanyia majaribio magari yanayojiendesha.Oktoba, kampuni inayounda magari yanayotumia umeme, Tesla, ilitangaza kwamba magari yake yote sasa yataundwa yakiwa na programu ya kuyawezesha kujiendesha bila kuwa na dereva.

Nchini Uingereza, gari la kujiendesha lilifanyiwa majaribio Milton Keynes majira ya joto, na majaribio zaidi yamepangiwa kufanyika London karibuni.

COMMENTS

Name

COMPUTER TIPS,8,IT Darasa,1,Makala,1,Maujanja ya Simu,22,Teknolojia,4,
ltr
item
WaiTech IT Solutions: Kampuni Ya Apple Kuunda Magari Yatakayojiendesha Yenyewe
Kampuni Ya Apple Kuunda Magari Yatakayojiendesha Yenyewe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAFykQs-DiWTnH7mSVJe7NiPoZ2YCxGlm7qnRCTMUZ0qAjQdGvIqqIwmXy7sNTsB65F-MgyMrYJXoaoeynw97r2OClNHIuJN78WIc8haatWJNytOU28jSrCOvs1rBxUkK-OtbvBiDowr_B/s1600/apple2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAFykQs-DiWTnH7mSVJe7NiPoZ2YCxGlm7qnRCTMUZ0qAjQdGvIqqIwmXy7sNTsB65F-MgyMrYJXoaoeynw97r2OClNHIuJN78WIc8haatWJNytOU28jSrCOvs1rBxUkK-OtbvBiDowr_B/s72-c/apple2.jpg
WaiTech IT Solutions
http://waitechs.blogspot.com/2016/12/kampuni-ya-apple-kuunda-magari.html
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/2016/12/kampuni-ya-apple-kuunda-magari.html
true
6135567013369675355
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy