Wapo watu wengi ambao wanapenda kubadili ukubwa wa maneno kwenye baadhi ya app zilizopo kwenye simu zao. Siku ya leo tutatumia whatsa...
Wapo watu wengi ambao wanapenda kubadili ukubwa wa maneno kwenye baadhi ya app zilizopo kwenye simu zao. Siku ya leo tutatumia whatsapp kama mfano maana ndio app inatumiwa na watu wengi.
Siku chache zilizopita tulijifunza jinsi ya kuongeza ukubwa wa maneno au kupunguza ukubwa wa maneno kwenye simu yako ya android. Leo tutaona jinsi ya kupunguza au kuongeza ukubwa maneno na muoenekano kwenye baadhi ya apps utakazo taka.
NOTE
Unaweza tumia huu mfano kubadili muonekano wa ukubwa wa vitu kwenye app yeyote kwenye simu yako ya android.
STEP 1
Hakikisha simu yako tayari ume root. Kama hauja root simu yako basi hautaweza kufanikiwa kupunguza au kuongeza ukubwa wa maneno kwenye whatsapp.STEP 2
Hakikisha kwenye simu yako tayari umeweka Xposed Installer. Xposed installer ina muonekano kama picha chiniSTEP 3
Hakikisha ume intsall App setting Module. Kama bado unaweza ku-download kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yakohttp://dl-xda.xposed.info/modules/de.robv.android.xposed.mods.appsettings_v29_70ccc5.apk
STEP 4
Baada ya kumaliza ku install App setting nenda kwenye xposed installer kisha nenda kwenye kipengele cha module na weka tick pembeni ya app settings kama picha chini kisha zima na kuwasha simu yakoSTEP 5
Hakikisha Xposed installer imeruhusiwa kupata root ya simu yako. Kwa kizungu ni kwamba "make sure xposed installer has been granted root access to system files". Kwa kifupi fungua super user app halafu hakikisha xposed installer inafanana kama picha chiniSTEP 6
Fungua App settings app kwenye simu yako na utapata muonekano kama picha chiniSTEP 7
Shuka chini mpaka utakapo ona Whastapp kama picha inavyo onekana chini.STEP 8
Bonyeza hicho kipengele cha Whatsapp kisha weka on kwenye neno setting kama picha inavyo onekana chiniSTEP 9
Ebdapo utafanikiwa basi utapata muonekano kama picha chiniSTEP 10
Kwenye sehemu iliyoandikwa DPI andika number yeyote mfano 320, 240... etc.. jinsi namba inavyozidi kuwa ndogo utakuwa unapunguza ukubwa wa maneno na muonekano wa whatsapp na jinsi unavyo andika number kubwa basi maneno na muonekano wa whatsapp utaonekana mkubwa.STEP 11
Baada ya kuandika number unayotaka kwenye sehemu ya DPI (mfano mimi nimeandika number 250),bonyeza sehemu yenye alama ya save na utapata muonekano kama picha chini kisha bonyeza okSTEP 12
Bonyeza sehemu iliyoandikwa MORE juu kulia kisha bonyeza kipengele kinachosema settingskama picha chiniSTEP 13
Bonyeza kipengele kinachosema FORCE STOP kama picha chiniSTEP 14
Zima simu yako kisha iwashe (restart). Nenda kafungue whatsapp na utaona muoenekano wa maneno na vitu vingene kwenye whatsapp vimebadilika. Mfano picha kushoto ni muonekano wa Whatsapp kabla sijaweka number kwenye DPI na picha kulia ni baada ya kuandika number 250 kwenye DPI.Kama umependa kazi zetu na unataka tuzidi kusonga mbele basi usiache kutu like facebook page yetu yenye jina la JaBi Technologies au wasiliana nasi kupitia whatsapp +255 713 515 059.
COMMENTS