Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknologia katika Page yetu na BLOG yetu ya Waitech Solutions. Miongoni mwa ta...
Habari, Ndugu
mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknologia katika Page yetu na BLOG yetu ya Waitech
Solutions.
Miongoni mwa tatizo linalowakabiri watumia wengi wa Smartphone ni
kusahau Password au Pattern ya simu zao, wengi huzani kwamba njia pekee ya
kuiondoa hii ni kuflash simu.
Katika makala hii tutajifunza njia rahisi ya kuondoa Password au Pattern
katika simu yako pasipo kuflash simu au kutumia software yoyote.
Kabla hatujaenda mbali ni vyema tukafahamu mambo ya msingi, katika
kufanya zoezi hili;-
ANGALIZO:-
1. Kwa kutumia njia hii, Vitu vyako kama nyimbo, picha, video, Apps na
data nyingine zilizohifanyiwa kwenye simu VITAFUTIKA maaana
simu huanza upya hivyo ni bora ukafahamu hilo mapema.
2. Pindi utakapo iruhusu simu kufanya factory reset, usiingilie aidha kwa kufosi kuiwasha au kuizima, hii inaweza kuua simu yako.
3. Tunashauri kufanya Backup ya vitu vyako mara kwa mara ili kuepuka
kutovipoteza hasa pale unaposahau password na kutumia njia hii kuiondoa.
Baada kuangalia mambo ya msingi turudi sasa kwenye somo letu, ili kuweza
kuondoa password au pattern kwenye simu yako unapaswa kufuata hatua zifuatazo:-
HATUA:-
1. Zima simu yako toa betri halafu lilirudishe.
2.a)Kama unatumia HUAWEI, VODAFONE AU TECNO bonyeza batani ya kuongezea
sauti na ya kuwashia kwa pamoja kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
b)Kama unatumia Samsung bonyeza batani ya kuwashia, kuongezea
sauti na home button kwa sekunde 15, kufanya hivyo
kutakuletea Recovery menu.
4. Bonyeza batani ya kuwashia kisha tumia batani ya kupunguzia sauti
kushuka mpaka kwenye delete all users data halafu bonyeza batani
ya kuwashia.
(kwa baadhi ya simu za TECNO na SONY, Bonyeza batani ya kuongezea sauti
kisha tumia batani ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data halafu bonyeza batani
ya kuongezea sauti).
5. Iache kwa muda kisha utaona neno Reboot now liko highlighted
bonyeza batani ya kuwashia kisha iache izime na iwake.
(kwa baadhi ya simu zitakuomba ukubali kufuta bonyeza batani ya kuwashia
kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza batani
ya kuwashia kisha iache izime na iwake).
kwa baadhi ya simu utatumia batani ya kuongezea sauti badala ya batani
ya kuwashia.
6. Mpaka hapo utakuwa umefanikisha kuondoa pattern bila ya kuflash simu
yako.
Natumaini hadi kufikia hapo, utakuwa na uelewa mzuri kuhusu namna ya
kuondoa Password au Pattern kwenye simu yako, endelea kuwa nasi kupitia blog
yetu ya Waitech Solutions ili uweze kujifunza mengi
yahusuyo teknolojia.
Usisahau ku-like Facebook Page yetu Waitech Solutions., unaweza ku-share na wengine makala hii.
COMMENTS