Njia Rahisi Ya Kutengeneza Nywila (Password) Kwa Usalama Wa Data Zako Ki-Digital

Mojawapo ya mambo ya msingi kabisa katika kuhakikisha unakuwa salama upande wa TEHAMA ni kuwa na nywila au password .   Nywila in...


Mojawapo ya mambo ya msingi kabisa katika kuhakikisha unakuwa salama upande wa TEHAMA ni kuwa na nywila au password.
 
Nywila inahitajika katika kila sehemu inayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano. Katika kompyuta yako. Katika programu unazozitumia ndani ya kompyuta yako. Katika tovuti. Katika mifumo ya taarifa ofisini. Katika nyumba tunazoishi, katika magari, n.k.

Lakini je ni nywila gani uitumie? Na ni kwa namna gani unaweza kuandaa nywila imara?

Katika makala hii utafahamu nini maana ya kuwa na nywila na dondoo kadhaa za kuandaa na kuwa na nywila imara.

Hebu kwanza tutatazame maana ya nywila. 

Nywila ni nini?
Nywila ni mkusanyiko wa mtiririko wa herufi na alama ambazo unazitumia ili kuweza kuruhusiwa kuingia katika mfumo wa ki-TEHAMA.
Kwa mfano unatumia nywila ili kuingia katika mfumo wa barua pepe. Hapo unakuwa na namba, tarakimu, herufi, na alama ambazo umezichanganya na kutengeneza nywila ambayo unaitumia kuingia.

Kwa namna hii nywila hutumika kama sehemu ya mfumo wa ulinzi wa vifaa, mfumo, na hata majengo. Karibu kila mahali, kila kitu na kila jambo sasa linahitaji mfumo imara wa ulinzi na usalama.
Nywila inahitajika ili kuwazuia watu au programu nyingine kuweza kuingia mahali wasiporuhusiwa. 

Ni sifa zipi za nywila imara?

Sifa ya kwanza kabisa ya nywila imara ni kwamba inatakiwa kuwa ndefu.

Hii ina maana kwamba inatakiwa kuwa ndefu kiasi cha kuzuia mtu mwingine kuweza kubashiri na kuunga unga na hatimaye kuipatia kwa urahisi.

Kama una nywila yenye namba 2 tu kwa mfano, 24, basi hapo ni kama hauna ulinzi wowote. Kwa sababu mtu anaweza kujaribu kuunda namba hizo kutokana na ukweli kwamba anaweza kuchagua kati ya 0 na 9.

Anaweza kujaribu 01, 22, 98, 25 na kuendelea. Mpaka atakapoipata.
Kwa hivyo hakikisha nywila yako inakuwa ndefu lakini ambayo unaweza kuikumbuka kwa urahisi.

Pili, nywila yako lazima iwe na mchanganyiko wa herufi, alama, na tarakimu.

Mchanganyiko wa mambo kama vile #, A, !, @, z, 4.
Na ndiyo maana unaona katika tovuti mbalimbali wanakudhibiti kuandika nywila ambayo ina mcganganyiko wa angalau tarakimu 1, herufi kubwa moja, na alama (character) 1.
Kwa mfano Naitw@12
Hii ina maana kubwa kiusalama. Mtu ambaye atajaribu kubashiri nywila hii atakuwa na wakati mgumu sana.

Tatu, hakikisha hautumii maneno ambayo yanapatikana katika kamusi au ambayo yanatokana na kubadili maana ya kitu au jambo fulani.

Kwa mfano, kama utakuwa na nywila mayo ambayo ni tafsiri ya neno mama kwa lugha ya kisukuma, basi mtu anaweza kuibashiri hasa kama anajua wewe ni msukuma.
Pia mtu anaweza kujaribu kuandika na kutumia nywila M$ney.

Kwa kuwa tunafahamu neno Money linahusisha alama ya $, mtu anaweza kujaribu bahati yake kwa kuweka alama hiyo katika mojawapo ya herufi za neno Money, kama ambavyo wewe mwenyewe ulivyofikiri.
Nywila kama hii itakuwa ni madhubuti pale tu itakapokuwa ndefu kwa mfano M$ney@_1788.

Nne na mwisho nywila yako lazima iwe rahisi kuikumbuka.

Hii haimaanishi kwamba tunapingana na dondoo tatu za nyuma. Hapa inamaanisha kwamba nywila yako lazima iwe rahisi kuikumbuka wewe mwenyewe pekee.

Hii ina maana kwamba andaa nywila ambayo imenadikwa kwa kufutana na kanuni ambayo wewe mwenyewe pekee ndiye unayeifahamu. Inatakiwa kuwa rahisi kuikumbuka lakini ngumu kuibashiri.

Kwanini unatakiwa kuwa na nywila?

Ndiyo, kwa wengine inaweza kuwa ni usumbufu kuandika nywila kila wanapotakiwa kutumia programu au mfumo wa TEHAMA. Lakini kuwa na nywila ni muhimu sana. Lengo na madhumuni ni:
Kuhakikisha kuwa inakuwa vigumu kwa mtu mwingine au programu shambulizi (brute force guessing) kufanikiwa kuingia kwenye akaunti au kompyuta yako.

Hii itawakatisha tamaa wadukuzi (hackers) ambao wanataka kuingilia mfumo wako. Hata kama wana utalaam wa hali ya juu na rasilimali za kuwawezesha kufanya hivyo, itawachukua muda mrefu sana kutimiza lengo lao.
Na mwishowe watakata tamaa, hasa ikizingatiwa kama data na taarifa wanazozitaka hazina thamani kubwa kulinganisha na gharama ya udukuzi huo.

Kumbuka kwamba kuwa na nywila ni muhimu sana, lakini pia ni sehemu ya mfumo mzima wa ulinzi na usalama.
Kwa hivyo kuwa na nywila (password) ngumu sana hakumaanishi uache kutumia akili ya kawaida katika kujilinda. Unatakiwa kuwa na mifumio mingine ya usalama kama vile antivirusi.
Hakikisha unafuata kanuni za usalama mahali pa kazi (security guidelines). Hakikisha unafanya kazi kulingana na sera ya usalama wa TEHAMA kazini kwako (ICT Security Policy).
Lakini jambo la msingi ni kuwa macho. Ni asilimia 20 tu ya usalama wa data, nyaraka na mambo mengine ya siri ndiyo hutegemea mambo kama password na mifumo.

Asilimia 80 iliyobaki inakuhusu wewe mwenyewe binafsi.

Imeandaliwa na JaBi Technologies

COMMENTS

Name

COMPUTER TIPS,8,IT Darasa,1,Makala,1,Maujanja ya Simu,22,Teknolojia,4,
ltr
item
WaiTech IT Solutions: Njia Rahisi Ya Kutengeneza Nywila (Password) Kwa Usalama Wa Data Zako Ki-Digital
Njia Rahisi Ya Kutengeneza Nywila (Password) Kwa Usalama Wa Data Zako Ki-Digital
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkC_1sldsT7lC9YLgfUZ2psZbsI_fQVjfdwgJyA8ZnSd2vGehf3ipDdGLFfjKleUj3_Dou_WiGKeM4QAc_kUUinbOPfTCoN_02nzr_xEd0NZb058-l7NNKarrVeV2mk5S3Tp6naugyARQ/s640/m3networks_password.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkC_1sldsT7lC9YLgfUZ2psZbsI_fQVjfdwgJyA8ZnSd2vGehf3ipDdGLFfjKleUj3_Dou_WiGKeM4QAc_kUUinbOPfTCoN_02nzr_xEd0NZb058-l7NNKarrVeV2mk5S3Tp6naugyARQ/s72-c/m3networks_password.jpg
WaiTech IT Solutions
https://waitechs.blogspot.com/2016/09/njia-rahisi-ya-kutengeneza-nywila.html
https://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/
http://waitechs.blogspot.com/2016/09/njia-rahisi-ya-kutengeneza-nywila.html
true
6135567013369675355
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy