Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknologia katika BLOG yetu ya Waitech Solutions. Bila shaka umewahi kumkwepa ...
Habari,
Ndugu mfuatiliaji
wa makala mbalimbali za teknologia katika BLOG yetu ya Waitech Solutions.
Bila shaka umewahi kumkwepa
mtu au kugombana na mtu kwa njia ya WhatsApp lakini ungependa kusoma ujumbe
aliokuandikia pasipo yeye kujua, au unahitaji kusoma ujumbe uliotumiwa pasipo
muhusika kufahamu.
Katika makala hii
tutajifunza namna ya kusoma ujumbe uliotumiwa WhatsApp bila “tick za blue”
kuonekana kwa mtumaji kama ujumbe umesomwa.
Tutaangalia njia mbili
tofauti:-
NJIA
YA KWANZA: Fuata hatua zifuatazo;-
1. Pindi utakapo pokea
meseji ya WhatsApp usiifungue kwanza.
2. Fungua Airplane mode na
uweke ON, ambayo itazuia matumizi ya data na meseji nyingine kuingia.
3. Kisha,, fungua WhatsApp
yako na usome meseji zako zote ambazo unataka mtumaji asione tick za blue mpaka
umalize kufanya yako.
4. Funga whatsApp yako
kabisa baada ya hapo nenda na utoe Airplane mode.
Hatakama utakuwa umezisoma
meseji hizo lakini tick mbili za blue hazitatokea kwa mtumaji.
5. Unaweza kuwasha data
yako na kuendelea na mambo yako mengine.
NJIA
YA PILI: Fuata hatua zifuatazo;-
1. Fungua WhatsApp yako,
2. Nenda sehemu ya
setting->account->privacy
3. Shuka chini mpaka kwenye
neno “read receipts” na uondoe alama ya
tick.
Njia hizi zitakusaidia
kusoma ujumbe wa mtu ambaye huitaji afahamu kuwa umesoma ujumbe wake, lakini
pia kama hauhitaji kuchati naye maana wengine hujisikia vibaya haswa pale wanapokuwa na ushahidi kuwa umesoma
meseji zao lakini hauwajibu.
ANGALIZO:-
Tumia njia hizi
kwa lengo la kujifunza na si vinginenyo, ukitumia kwa lengo baya sisi
hatutahusika, kazi yetu ni kukuelimisha.
Endelea kuwa nasi kupitia blog yetu ya Waitech Solutions ili uweze kujifunza mengi yahusuyo teknolojia.
Usisahau ku-like facebook page yetu Waitech Solutions.
COMMENTS