Barua pepe ni mojawapo ya njia za mawasiliano ya kielektroniki zenye manufaa sana kwa jamii. Njia hii ya mawasiliano inatumika na watu ...
Barua pepe ni mojawapo ya njia za mawasiliano ya kielektroniki zenye manufaa sana kwa jamii. Njia hii ya mawasiliano inatumika na watu binafsi, serikali pamoja na mashirika mbalimbali kwa manufaa makubwa! Watumiaji wa huduma hii mara kwa mara wamekua wanapata usumbufu kutoka aidha kwa watu wenye anuani zao za barua pepe, au kutoka kwa makampuni ambayo hutuma ujumbe wa barua pepe kwenye akaunti za watu aidha kwa kupenda au kwa kutokupenda! Katika makala haya nitakuelekeza namna ya kuzuia barua pepe kutoka kwa watu/mashirika wanaokusumbua/yanaokusumbua.
HATUA:
KWA WATUMIAJI WA GMAIL
i) Ingia katika akaunti yako (Login into your account).
ii) Baada ya kuingia ndani, angalia juu kabisa upande wa kulia utaona icon ya gia, bonyeza pale, menyu itashuka chagua settings.
iii) Baada ya kufunguka, click link ya filter.
iv) Bonyeza create a new filter.
v)Jaza fomu kulingana na vipengele vilivyopo, mfano ingiza anuani ya email unayotaka kuzuia email zake kukufikia. mimi nimejaza kama mfano tu kukuelekeza namna ya kufanya! Bonyeza Create filter with thiskuendelea mbele.
pia unaweza kuzuia email/barua pepe zinazohostiwa na domain fulani, mfano andika *@abc.com .
vi)Tiki kibox cha Delete it au chochote unachotaka kitokee halafu malizia kwa kubonyeza link Create filter.
vii) Utajulishwa kuwa kichujio/filter uliyoseti imekubali!
MWISHO:
Katika machapisho yajayo nitakujuza namna ya kublock barua pepe ambazo huzitaki katika domain nyingine! Elimika nayo!!
COMMENTS