Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknolojia katika blogu hii ya Waitech Solutions. Katika makala hii fupi, tutakuo...
Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknolojia katika blogu hii ya Waitech Solutions.
Katika makala hii fupi, tutakuonyesha matumizi ya “Delete” katika kompyuta na namna inavyoweza kutumika hasa kwa watumiaji wa teknolojia hiyo.
Moja ya operation ambayo inafanyika mara kwa mara katika matumizi ya kompyuta ni delete. Delete hufanya kazi ya kufuta file lililopo katika sehemu au location katika kompyuta.
Kuna namna mbili ambazo unazoweza kutumia kufuta file katika kompyuta:
(1) Katika namna hii ya kwanza unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kitufe katika keyboard kilichoandikwa delete au unabofya kitufe cha kulia cha mouse na kuchagua delete.
Mara baada ya kubofya, file litandolewa kutoka sehemu iliyopo kwenda katika recycle bin. Unaweza kulirudisha file ikiwa umelifuta kwa makosa kwa kubofya na kuchagua restore. Ikiwa pia unataka ulifute katika recycle bin basi rudia hatua za kawaida za kufuta file kama nilivyoelekeza hapo juu.
(2) Katika namna hii ya pili unachagua file unalotaka kulifuta kisha unabofya kwa pamoja (simultaneously) vitufe katika keyboard shift na delete.
Mara baada ya kubofya, file litaondolewa kutoka sehemu iliyokuwa lakini halitapelekwa katika recycle bin. Hapa unakuwa hauwezi kulirudisha file lilipokuwa. Hii hufahamika kama kudelete permanently.
Unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu makala hii kwa ajili ya kupata maarifa.
COMMENTS