Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknologia katika Page yetu na BLOG yetu ya Waitech Solutions. Watu wengi wamekuwa ...
Habari, Ndugu mfuatiliaji wa makala mbalimbali za teknologia katika Page yetu na BLOG yetu ya Waitech Solutions.
Watu wengi wamekuwa
wakijiuliza kama inawezekana kuwa na WhatsApp
akaunti mbili katika simu moja, yawezekana nawe ukawa mmoja wapo.
Kupitia makala hii,
utajifunza namna ya kutumia WhatsApp akaunti mbii kwenye simu yako.
Kufahamu zaidi, fuata hatua
zifuatazo:-
HATUA:-
1. Download App inayoitwa “parallel space” kwenye play store.
2. Kama simu yako ni line moja
basi weka line nyingine ambayo unataka iwe Whatsapp yako ya pili.
3. Install application uliyo
download kwenye hatua ya 1(parallel space)., kisha ifungue.
4. Baada ya kuifungua, Utakapofika
kwenye kipengele kinachotaka kuweka namba ya simu hapo utaweka namba yako ya
pili ili uweze kuwa na WhatsApp mbili.
5. Utaendelea na hatua za
kawaida kama ulivyojiunga na WhatsApp ya kwanza.
Mpaka hapo utakuwa
umefanikiwa kuweka na kuanza kutumia WhatsApp
akaunti mbili kwenye simu moja.
MUHIMU:-
Njia hii pia yaweza tumika kwa kuiwezesha simu kuwa na akaunti mbili za mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, Instagram, Messenger, Snapchat n.k
Endelea kuwa nasi kupitia blog yetu ya Waitech Solutions ili uweze kujifunza mengi yahusuyo teknolojia.
Unaweza ku-share na wengine makala hii.
COMMENTS