Katika Somo hili utajifunza kuhusu Kampuni ya Microsoft na Historia fupi ya waanzilishi wake na namna walivyofanikiwa. Kuhusu kampu...
Katika Somo hili utajifunza
kuhusu Kampuni ya Microsoft na Historia fupi ya waanzilishi wake na namna walivyofanikiwa.
Kuhusu kampuni ya Microsoft
Kampuni ya Microsoft ni
kampuni ambayo hutengeneza programu za kompyuta kwa ajili ya watumiaji wa
kompyuta duniani kote. Ilianzishwa mnamo mwaka 1975 na Bill Gates kwa
kushirikiana na Paul Allen.
Programu ambazo
hutengenezwa na kampuni hii ni pamoja na Windows, Microsoft office (kama vile,
Microsoft word, Powerpoint, Publisher n.k), internet exproler (Programu ya
kuingilia katika mtandao wa intaneti), websaiti ya Microsoft ijulikanayo kama
Microsoft Network (MSN) ambayo hutumika kuingilia kwenye mtandao wa intaneti
n.k.
Baadhi ya programu za
Microsoft kama vile mfumo wa Window wa uchakatuaji (Windows operating system)
huwa zimekwisha ingizwa mara mtu ananunuapo kompyuta. Mtu aweza kununua na
kuingiza nyingine kulingana na uhitaji wake.
Microsoft Windows ni nini?
Microsoft Windows ni mfomu
laini wa uchakatuaji (operating system) ambao ni wa msingi ambao hufanya
kompyuta kufanya kazi na kuruhusu program nyingine nazo kufanya kazi.
Aina za Windows
zinazotumika ni Windows XP au Windows 7 na Windows 8.1 ambalo ni toleo la hivi
karibuni.
Microsoft ofisi ni seti
(mkusanyiko) ya program ambazo hutumika katika kompyuta kuwawezesha watu
kuandika dokumenti. Mfano Microsoft Word na Microsoft Excel ambayo hukuwesha
kutengeneza mahesabu na majedwali na Microsoft PowerPoint ambayo hukuwezesha
kuandaa mawasilisho (presentations).
Kwakuwa programu hizi
hufanya kazi katika kompyuta, sehemu inayofuata inalenga kukupa ufahamu juu ya
sehemu za kompyuta (hasa za nje) na zinavyofanya kazi.
Kuhusu waanzilishi wa
kampuni ya Microsoft
Kampuni ya Microsoft
ilianzishwa na marafiki wawili; William Henry Bill Gates na Paul
Gardner Allen
William Henry Bill Gates alizaliwa
tarehe 28/10/1955 huko Seattle, Washington Marekani.
Bwana Bill Gates alianza kuonesha mapenzi makubwa kwa teknolojia akiwa na umri
wa miaka 13 ambapo alianza kutengeneza programu
za kompyuta.
Kupitia ujuzi wake wa kutengeneza programu za kompyuta na ujuzi wa mikakati ya kibiashara yeye pamoja na rafiki yake Paul Allen walijenga biashara kubwa ya programu za kompyuta iitwayo Microsoft.
Kupitia ujuzi wake wa kutengeneza programu za kompyuta na ujuzi wa mikakati ya kibiashara yeye pamoja na rafiki yake Paul Allen walijenga biashara kubwa ya programu za kompyuta iitwayo Microsoft.
Biashara hii hatimaye
ilimfanya Bill Gates kuwa mmoja wa matajiri wakubwa ulimwenguni. Alisoma katika
Shule ya Lakeside kati ya mwaka 1967 na 1973 kisha akasoma katika chuo
cha Harvard Mnamo mwaka 1973 mpaka 1975
Huko Marekani. Ana mke aitwaye Melinda Gates na watoto watatu; Jennifer
Katharne Gates, Rory John Gates na Adele Gates.
Paul Gardner Allen ni mfadhili wa Kimarekani, mwekezaji na mbunifu. Huyu ni rafiki yake Bill Gates na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft. Alizaliwa January 21, 1953 Katika mji wa Seattle, Washington Marekani. Alisoma katika shule moja na Bill Gates iitayo Seatle na baadae alijiunga na chuo kikuu cha Serikali cha Washington (Washington State University) ambapo hakumaliza masomo yake badala yake akakimbilia Boston ambapo alipata ajira katika kampuni iitwayo Honeywell.
Baada ya hapo Bill Gates aliungana naye wakaiendeleza safari ya ubunifu na hatimaye wakaanza biashara kubwa ya program za kompyuta iitwayo Microsoft.
Asante,,
Usikose kufuatilia Somo la Pili katika Blog hii au kupitia ukurasa wetu wa Facebook uitwao WaiTech Solutions.
COMMENTS